Maswali ya kawaida

Kama swali lako halipo hapa, tuandikie WhatsApp — tunajibu haraka.

Inachukua muda gani kupata kadi zangu?
Mfano wa kwanza wa design unaupata ndani ya saa 24 baada ya kutuma taarifa za tukio. Baada ya kuidhinisha design, kadi zote za wageni zinakuwa tayari ndani ya siku 1 hadi 3, kutegemea idadi.
Nina wageni 500. Mnaweza?
Ndiyo. Mfumo wetu unatengeneza kadi kwa wingi — wageni 50 au 1,000 ni kazi ile ile. Kila mmoja anapata kadi yake yenye jina na namba yake.
Je, QR inahitaji internet mlangoni?
Ukurasa wa kuhakiki unahitaji internet kufunguka mara ya kwanza. Baada ya hapo unafanya kazi hata mtandao ukiwa dhaifu. Pia tunakupa orodha ya wageni inayotafutwa kwa namba ya kadi kama akiba, na orodha ya kuchapisha ya karatasi.
Nikitaka kubadilisha jina au namba ya mgeni baada ya kutuma?
Inawezekana. Marekebisho baada ya kadi kuidhinishwa ni TZS 1,600 kwa kadi. Kabla ya kuidhinisha, marekebisho ni bure.
Mnatuma vipi kadi kwa wageni?
Kwa WhatsApp na SMS moja kwa moja kutoka kwenye rejista yako. Ujumbe unaanza kwa jina la mgeni na kadi yake inaambatanishwa. Hakuna kazi ya kusambaza wewe mwenyewe.
Malipo yanafanyikaje?
Asilimia 50 kuanza kazi, na asilimia 50 kabla ya kutuma kadi kwa wageni. Tunapokea M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, HaloPesa na benki.
Je, mnafanya kadi za kuchapisha pia?
Ndiyo. Design ile ile inachapishwa kwa karatasi ya ubora kwa TZS 3,700 kwa kadi. Wengi huchanganya: kadi za kidijitali kwa wageni wote, na kadi za kuchapisha kwa wazee na wageni maalum.
Mnafanya kazi nje ya Dar es Salaam?
Ndiyo. Kadi za kidijitali zinafanya kazi popote Tanzania na nje ya nchi. Kwa huduma ya timu ya kuhakiki mlangoni (Luxury), tunapanga kwa makubaliano kwa matukio ya nje ya Dar.
Je, mnahifadhi taarifa za wageni wangu?
Rejista yako ni yako. Hatutumii namba za wageni wako kwa kitu kingine chochote, na tunazifuta baada ya tukio ukitaka.

Bado una swali?

Tuandikie WhatsApp — tunajibu ndani ya dakika chache wakati wa kazi.