Kila kitu unachohitaji kuanzia kubuni kadi hadi kuhakiki mgeni mlangoni siku ya tukio.
Kila mgeni anapata kadi yenye jina lake, namba ya kadi na aina (Single au Double). Hakuna kadi mbili zinazofanana — ndiyo maana mlangoni hakuna mgogoro.
Kila kadi ina QR yake. Ukurasa wa kuhakiki unafunguliwa kwenye simu ya mtu wa mlangoni — anascan, anaona jina, na mgeni anaingia. Hakuna kuingia mara mbili.
Ukurasa binafsi kwa kila mgeni: ramani ya kufika, ratiba ya siku, countdown, dress code, kuweka kwenye kalenda, na RSVP.
Tunatuma kadi, vikumbusho na ujumbe wa asante moja kwa moja kwa kila mgeni. Ujumbe unaanza kwa jina lake, si “Habari mgeni”.
Excel yenye majina, namba za simu, namba za kadi, ahadi na michango. Unajua nani kapata kadi, nani hajapata, na nani kaingia.
Design ile ile ya kidijitali inachapishwa kwa karatasi ya ubora. Kwa wageni wanaopenda kadi ya mkononi.
Video fupi ya mwaliko kwa Instagram, WhatsApp Status na TikTok — yenye majina yenu, tarehe na mahali.
Nani alihudhuria, nani hakuja, saa ngapi walifika. Ripoti kamili ndani ya siku moja baada ya tukio.
Matukio
Tuambie kuhusu tukio lako, tukupe ushauri na bei ndani ya saa chache.