Mialiko · Kadi · QR
Tunatengeneza kadi ya mwaliko yenye jina la mgeni, namba yake na QR ya kipekee — inatumwa moja kwa moja WhatsApp, na mlangoni inahakikiwa kwa sekunde.
Tunachofanya
Si picha moja unayosambaza kwa wote. Ni kadi ya mtu mmoja mmoja, yenye jina lake na namba yake.
Kila kadi inabeba jina la mgeni kama anavyotaka kuitwa, namba ya kadi, na aina yake — Single au Double.
Kila kadi ina QR yake pekee. Mlangoni mnaiscan, mnaona jina na aina ya kadi, na mnamruhusu mara moja.
Tunatuma kadi kwa WhatsApp na SMS moja kwa moja kwa kila mgeni — huna kazi ya kusambaza wewe.
Ukurasa binafsi wenye ramani, ratiba, countdown na RSVP — mgeni anafungua kwa mbofyo mmoja.
Orodha kamili ya nani kapata kadi, namba ngapi, na nani kaingia siku ya tukio. Yote kwenye Excel.
Ukitaka kadi halisi za mkononi, tunazichapisha kwa ubora ule ule wa design ya kidijitali.
Inavyofanyika
Jina la tukio, tarehe, mahali, saa, na orodha ya wageni wako.
Ndani ya saa 24 unapata design ya kadi. Unarekebisha hadi uridhike.
Kila mgeni anapokea kadi yake WhatsApp na SMS, yenye jina lake.
Siku ya tukio mnascan QR. Baada ya tukio unapata ripoti ya waliohudhuria.
Mifano ya kadi
Harusi, send-off, kitchen party, nikah, maulidi, mahafali, komunio, kipaimara na sherehe za kuzaliwa.




Kazi halisi
Kadi 312 za kidijitali, kila moja na jina la mgeni na QR yake. Mialiko, vikumbusho na kadi ya asante — zote zilitumwa kwa WhatsApp na SMS moja kwa moja kutoka kwenye rejista.
Jaza fomu fupi na upate bei yako papo hapo, au tuandikie WhatsApp sasa hivi.