Mialiko · Kadi · QR

Kila mgeni apate kadi yake mwenyewe

Tunatengeneza kadi ya mwaliko yenye jina la mgeni, namba yake na QR ya kipekee — inatumwa moja kwa moja WhatsApp, na mlangoni inahakikiwa kwa sekunde.

1,600/=Kuanzia kwa kadi
24 saaMfano wa kwanza
QRKuhakiki mlangoni
Mfano wa kadi ya mwaliko wa harusi Mfano wa kadi ya mwaliko wa send-off

Tunachofanya

Mwaliko unaokaa mkononi mwa mgeni

Si picha moja unayosambaza kwa wote. Ni kadi ya mtu mmoja mmoja, yenye jina lake na namba yake.

Kadi binafsi

Kila kadi inabeba jina la mgeni kama anavyotaka kuitwa, namba ya kadi, na aina yake — Single au Double.

QR ya kuhakiki

Kila kadi ina QR yake pekee. Mlangoni mnaiscan, mnaona jina na aina ya kadi, na mnamruhusu mara moja.

Kutuma WhatsApp

Tunatuma kadi kwa WhatsApp na SMS moja kwa moja kwa kila mgeni — huna kazi ya kusambaza wewe.

Tovuti ya mwaliko

Ukurasa binafsi wenye ramani, ratiba, countdown na RSVP — mgeni anafungua kwa mbofyo mmoja.

Rejista ya wageni

Orodha kamili ya nani kapata kadi, namba ngapi, na nani kaingia siku ya tukio. Yote kwenye Excel.

Kadi za kuchapisha

Ukitaka kadi halisi za mkononi, tunazichapisha kwa ubora ule ule wa design ya kidijitali.

Inavyofanyika

Kutoka oda hadi mlangoni

Unatuma taarifa

Jina la tukio, tarehe, mahali, saa, na orodha ya wageni wako.

Tunakupa mfano

Ndani ya saa 24 unapata design ya kadi. Unarekebisha hadi uridhike.

Tunatuma kadi

Kila mgeni anapokea kadi yake WhatsApp na SMS, yenye jina lake.

Mnahakiki mlangoni

Siku ya tukio mnascan QR. Baada ya tukio unapata ripoti ya waliohudhuria.

Mifano ya kadi

Kadi kwa kila tukio

Harusi, send-off, kitchen party, nikah, maulidi, mahafali, komunio, kipaimara na sherehe za kuzaliwa.

Kadi ya mwaliko wa harusi
Harusi
Kadi ya mwaliko wa send-off
Send-off
Kadi ya mwaliko wa kitchen party
Kitchen party
Kadi ya mwaliko wa sherehe ya kuzaliwa
Sherehe ya kuzaliwa

Kazi zetu zote

Kazi halisi

Harusi ya Isaack & Lucy

Kadi 312 za kidijitali, kila moja na jina la mgeni na QR yake. Mialiko, vikumbusho na kadi ya asante — zote zilitumwa kwa WhatsApp na SMS moja kwa moja kutoka kwenye rejista.

312Kadi binafsi
287Kadi za asante
100%Zilifika
QRMlangoni
Kadi ya harusi Kadi ya kitchen party

Tuandalie mwaliko wako

Jaza fomu fupi na upate bei yako papo hapo, au tuandikie WhatsApp sasa hivi.