Huduma zetu

Kila kitu unachohitaji kuanzia kubuni kadi hadi kuhakiki mgeni mlangoni siku ya tukio.

Kadi ya kidijitali binafsi

Kila mgeni anapata kadi yenye jina lake, namba ya kadi na aina (Single au Double). Hakuna kadi mbili zinazofanana — ndiyo maana mlangoni hakuna mgogoro.

QR ya kuhakiki mlangoni

Kila kadi ina QR yake. Ukurasa wa kuhakiki unafunguliwa kwenye simu ya mtu wa mlangoni — anascan, anaona jina, na mgeni anaingia. Hakuna kuingia mara mbili.

Tovuti ya mwaliko

Ukurasa binafsi kwa kila mgeni: ramani ya kufika, ratiba ya siku, countdown, dress code, kuweka kwenye kalenda, na RSVP.

Kutuma WhatsApp na SMS

Tunatuma kadi, vikumbusho na ujumbe wa asante moja kwa moja kwa kila mgeni. Ujumbe unaanza kwa jina lake, si “Habari mgeni”.

Rejista ya wageni

Excel yenye majina, namba za simu, namba za kadi, ahadi na michango. Unajua nani kapata kadi, nani hajapata, na nani kaingia.

Kadi halisi za kuchapisha

Design ile ile ya kidijitali inachapishwa kwa karatasi ya ubora. Kwa wageni wanaopenda kadi ya mkononi.

Video ya mwaliko

Video fupi ya mwaliko kwa Instagram, WhatsApp Status na TikTok — yenye majina yenu, tarehe na mahali.

Ripoti baada ya tukio

Nani alihudhuria, nani hakuja, saa ngapi walifika. Ripoti kamili ndani ya siku moja baada ya tukio.

Matukio

Tunahudumia sherehe zote

Harusi

Send-off

Kitchen party

Nikah

Maulidi

Iftar / Ramadhani

Mahafali

Komunio

Kipaimara

Sherehe ya kuzaliwa

Baby shower

Mikutano ya kampuni

Huduma gani unaihitaji?

Tuambie kuhusu tukio lako, tukupe ushauri na bei ndani ya saa chache.